Isaiah 10:5-13

Hukumu Ya Mungu Juu Ya Ashuru

5 a“Ole kwa Ashuru, fimbo ya hasira yangu,
ambaye mkononi mwake ana rungu ya ghadhabu yangu!
6 bNinamtuma dhidi ya taifa lisilomjua Mungu,
ninamtuma dhidi ya taifa linalonikasirisha,
kukamata mateka na kunyakua nyara,
pia kuwakanyaga chini kama matope ya barabarani.
7 cLakini hili silo analokusudia,
hili silo alilo nalo akilini;
kusudi lake ni kuangamiza,
kuyakomesha mataifa mengi.
8 dMaana asema, ‘Je, wafalme wote
si majemadari wangu?
9 eJe, Kalno hakutendwa kama Karkemishi?
Hamathi si kama Arpadi,
nayo Samaria si kama Dameski?
10 fKama vile mkono wangu ulivyotwaa falme za sanamu,
falme ambazo vinyago vyao vilizidi vile vya Yerusalemu na Samaria:
11 gje, nisiishughulikie Yerusalemu na sanamu zake
kama nilivyoshughulikia Samaria na vinyago vyake?’ ”
12 hBwana atakapokuwa amemaliza kazi yake yote dhidi ya Mlima Sayuni na Yerusalemu, atasema, “Nitamwadhibu mfalme wa Ashuru kwa ajili ya majivuno ya ukaidi wa moyo wake na kutazama kwa macho yenye dharau.” 13 iKwa kuwa anasema:

“ ‘Kwa nguvu za mkono wangu nimefanya hili,
kwa hekima yangu, kwa sababu nina ufahamu.
Niliondoa mipaka ya mataifa,
niliteka nyara hazina zao,
kama yeye aliye shujaa
niliwatiisha wafalme wao.
Copyright information for SwhNEN